Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wanaichukulia kwa uzito mkubwa michezo yote iliyobaki ili kuhakikisha wanapata ushindi
Kocha huyo raia wa Tunisia amesema kila mchezo uliobaki kwao ni fainali, watapambana kuhakikisha wanapata matokeo
Yanga iliondoka mapema leo jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Mtwara ambako wataweka kambi kabla ya kuelea Lindi wanakokabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa Jumamosi, uwanja wa Majaliwa
"Kila mchezo kwetu ni fainali, tunashuka dimbani kupambana kusaka ushindi lakini lazima tuwaheshimu wapinzani wote tunaokutana nao"
"Tunajiandaa vizuri kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya Namungo FC, tunafanyia kazi mapungufu yetu na kujiimarisha kwenye safu ya ushambuliaji, viungo pamoja na mabeki ili kwenda kutafuta matokeo chanya katika mchezo huo," alisema Nabi
Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 57 nyuma ya watani zao Simba wanaongoza wakiwa na alama 61