Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina aliondoka wiki iliyopita kwenda kwao nchini Zambia kuhudhuria sherehe ya kifamilia.
Lwandamina anatarajiwa kurejea mapema kabla ya Yanga kuivaa Mbao FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 12.
Kwa sasa kikosi cha Yanga kiko chini ya kocha msaidizi Shedrack Nsajigwa ambaye kesho ataongoza mapambano ya kukabiliana na Reha FC katika mchezo wa kombe la FA.
Aidha kulingana na Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten beki mpya Fiston Kayembe aliyepewa ruhusa kwenda kwao DRC kushughulikia matatizo ya kifamilia anatarajiwa kurejea mwanzoni mwa wiki.

ADVERTISE HERE