Kikosi cha Yanga kimeondoka mkoani Mtwara tayari kwa safari ya Dodoma wanakokabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa keshokutwa Jumatano katika uwanja wa Jamhuri
Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Namungo Fc katika mchezo ambao Wananchi walinyimwa bao halali, wamesahau matokeo hayo na sasa wanaelekeza nguvu zao kwa mchezo unaofuata mkoani Dodoma
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema bado hawajakata tamaa, wataendelea kupambana mpaka mwishoni mwa msimu hesabu zao zikiwa bado katika ubingwa
ADVERTISE HERE