Yanga imerejea jijini Dar es salaam mapema leo wakitokea mkoani Mtwara baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc uliopigwa Ruangwa, Lindi na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Keshokutwa Jumatano Wananchi watakuwa mkoani Dodoma kwa ajili ya mchezo mwingine wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania
Huu ni mchezo ambao Yanga inazihitaji alama zote tatu ili kuendelea kuwapa presha watani zao Simba ambao juzi walikumbana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Kaizer Chiefs katika mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa
Yanga imeshuka dimbani mara 28, wamesalia na michezo sita, miwili ikiwa nje ya Jiji
Baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania, Wananchi watabaki na mchezo mmoja tu nje ya Dar es salaam ambao ni dhidi ya Dodoma Jiji
Mchezo huo utakuwa wa mwisho kukamilisha msimu huu mwezi Julai