Dalili za Yanga imara zinaonekana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 May 2021
Dalili za Yanga imara zinaonekana

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi, jana alikiongoza kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma

Mabao ya Yacouba Songne na Tuisila Kisinda, yalitosha kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu ambazo zinawafanya wafikishe alama 61 wakitofautiana mabao tu na watani zao Simba

Huo ulikuwa mchezo wa nne kwa kocha Nabi ambaye alikabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi cha Yanga mwezi uliopita

Ni ushindi wake wa pili, ukiwa wa kwanza kwenye ligi, mchezo mwingine alioshinda ni kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons

Pengine ulistahili kuwa ushindi wake wa tatu kama sio zile figisu za waamuzi zilizofanywa kule Ruangwa katika mchezo dhidi ya Namungo Fc

Yapo maboresho yanayoonekana kwenye kikosi cha Yanga chini yake, vijana wanashambulia kwa kasi, wanatengeneza nafasi na hata kwenye kujilinda umakini umeongezeka

Wakati anakabidhiwa majukumu, Nabi aliahidi kuwa ataifanya Yanga kuwa moja ya timu bora barani Afrika, anachohitaji ni muda wa kuifanya kazi hiyo

Taratibu timu imeoanza kuonyesha utofauti, ile ari na upambanaji waliokuwa nao wachezaji kwenye duru ya kwanza imeanza kuonekana tena

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’