Jana klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wake Dk Mshindo Msolla ametangaza Mkutano Mkuu wa Wanachama wa mwaka utakaofanyika Juni 27 kwa mujibu wa ibara ya 20 ya katiba ya Yanga
Yanga imewataka wanachama wenye kadi ambazo hazijalipiwa kuhakikisha wanalipia mapema ili kupata haki ya kushiriki mkutano huo
Mkutano huo utabeba ajenda mbalimbali lakini kubwa ni mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji
Hii inatarajiwa kuwa ajenda itakayobeba Mkutano kwani ndilo hitaji la Yanga wakati huu
Wanachama wanapaswa kujielimisha na kuifahamu vyema rasmi mabadiliko
Elimu itatolewa kwa Wanachama kupitia Matawi yao ili kuhakikisha wanaelewa kile watakapopaswa kufanya kwenye Mkutano huo
Kwani wao ndio watakoamua hatma ya muundo mpya wa mfumo wa uendeshaji wa Yanga
Wananchi wanataka kuona Mabadiliko ya kweli ambayo yataipeleka Yanga awamu nyingine