Mabingwa wa mara tatu mfululizo ligi kuu ya Vodacom, Yanga wametinga mzunguuko wa tatu wa kombe la FA baada ya kuilza Reha FC mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Jumapili, Disemba 24 katika dimba la Uhuru.
Reha FC timu kutoka wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam ambayo inashiriki daraja la pili ilitoa upinzani mkali kwa mabingwa hao wa kihistoria wa soka la Tanzania.
Milango ilikuwa migumu hadi timu zinakwenda mapumziko.
Kwenye kipindi cha pili Yanga iliingia kwa nguvu kusaka ushindi huku Reha FC ikitumia mbinu ya kulinda na kushambulia kwa kushitukiza.

Hata hivyo mlinda lango wa timu hiyo ndiye aliyekuwa shujaa wa mchezo kwani alizuia michomo mingi ya washambuliaji wa Yanga.
Hata hivyo alishindwa kuzuia mpira uliopigwa kifundi na Pius Buswita kwenye dakika ya 83 na kuiandikia Yanga bao la kuongoza.
Wakati Reha FC wakijaribu kufanya mashambulizi kusaka bao la kusawazisha, Amissi Tambwe alizima ndoto zao za kutinga mzunguuko wa tatu baada ya kuifungia Yanga bao la pili kwenye dakika ya 86, akiunganisha kwa kichwa mpira mrefu wa Cannavaro.

Hakika kurejea kwa Tambwe ambaye leo alikabwa sana, kumeiongezea Yanga nguvu ya ushambuliaji kwani ni mchezaji ambaye hahitaji nafasi nyingi ili aweze kufunga.
Kiungo Papi Kabamba Tshishimbi ameendelea kuipendezesha Yanga kwa soka lake la umakini na kuvutia huku Gadiel Michael akimpa ujumbe Mwinyi Haji kuwa itamlazimu afanye kazi ya ziada ili aweze kumpoka namba.
Raphael Daudi akishirikiana na Tshishimbi walilikamata haswa dimba huku Buswita akipanda mbele kumsaidi Amissi Tambwe.
Yanga iliwakilishwa na;
1. Youthe Rostand
2. Juma Abdul
3. Gadiel Michael
4. Andrew Vicent
5. Nadir Haroub
6. Papi Kabamba Tshishimbi
7. Yusuph Mhilu
8. Raphael Daudi
9. Amissi Tambwe
10. Pius Buswita
11. Emanuel Martin/Said Musa (70)

ADVERTISE HERE