Ofa zimeendelea kumiminika Jangwani kwa ajili ya kiungo Mukoko Tonombe aliyetua Yanga kutoka klabu ya AS Vita mwaka jana
Baada ya Kaizer Chiefs kukwama, klabu ya Horoya kutoka nchini Guinea imejitosa kumuwania kiungo huyo anayecheza timu ya Taifa ya DR Congo
Inaelezwa Horoya wako tayari kutoa kitita cha zaidi ya dola 200,000 ambazo ni zaidi ya Milioni 464 fedha za Kitanzania
Mwaka juzi Horoya walimsajili Heritier Makambo na sasa wamerejea tena kumtaka Mukoko
Hata hivyo haitakuwa rahisi kwa Yanga kumuachia Mukoko wakati huu ambao wanaimarisha kikosi
Mukoko ni mchezaji muhimu sana kwa wakati huu, haitakuwa rahisi kupata mchezaji aina yake kwa haraka
ADVERTISE HERE