Azam Media na TFF leo wamesaini mkataba wa haki za matangazo ya ligi kuu mwenye thamani ya Tsh Bilioni 225.6 ukiwa ni mkataba wa miaka 10
Mkataba huo utavinufaisha vilabu kwani mgawanyo wa mapato utaongezeka miongoni mwa timu zote washiriki
Moja ya mambo muhimu ni kuongezeka kwa bonus ambapo kwa misimu mitatu ijayo, bingwa wa ligi kuu atakusanya kitita cha Tsh Milioni 500
Mshindi wa pili ataondoka na jumla ya Tsh Milioni 250, mshindi wa tatu Tsh Milioni 225 na mshindi wa nne Tsh Milioni 200
Pia mgawanyo wa fedha utakuwa ukiongezeka kila msimu

Haya ni mapinduzi makubwa, kwa hakika vilabu vitaanza kuona matunda ya kushiriki ligi kuu
Lakini muhimu zaidi ni kwa TFF kuhakikisha wanaboresha uendeshaji wa ligi ili timu zishindane katika usawa
ADVERTISE HERE