Baada ya kauli iliyotolewa jana na Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli kuhusu kutotambua ratiba ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopangwa kupigwa Julai 03, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema hiyo haikuwa kauli ya klabu
Kumekuwa na mjadala mkali uliowaibua viongozi wa Bodi ya Ligi Steven Mguto (Mwenyekiti) na Mtendaji Mkuu Almasi Kasongo ambao wamesema kama Yanga haitapeleka timu uwanjani Julai 03 wataadhibiwa kama kanuni zinavyoelekeza
Mfikirwa amesema kauli iliyotolewa na Bumbuli yalikuwa ni maoni yake binafsi,Β msimamo wa klabu watauweka hadharani karibuni
"Kauli hiyo haikuwa kauli rasmi ya klabu. Msimamo wetu kuhusu mchezo huo tutautoa. Kwa sasa ieleweka hivyo," alisema Mfikirwa
Wakati akihojiwa na Azam TV, Bumbuli alisema kuwa kwa sasa Yanga inajiandaa kwa ajili ya kukamilisha mechi nne za VPL pamoja na kombe la FA na kuwa mchezo dhidi ya Simba uliopangwa kupigwa Julai 03, uliopaswa kuchezwa Mai 08, hawautambui