Lamine arejeshwa kikosini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jun 2021
Lamine arejeshwa kikosini

Baada ya uongozi wa Yanga kumaliza sintofahamu iliyokuwa ikimkabili nahodha wa Yanga Lamine Moro, beki huyo kutoka Ghana ameungana na wachezaji wenzake katika kambi ya timu hiyo kuendelea na maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara zilizobakia

Awali ilielezwa Lamine amesimamishwa baada ya kutuhumiwa kufanya utovu wa nidhamu wakati timu ikiwa kambini mkoani Mtwara kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema baada ya kukutana na nyota huyo na baadae benchi la ufundi, wamemaliza sintofahamu iliyojitokeza awali

Mfikirwa alisema uongozi ulilazimika kulifanyia kazi suala hilo kwa sababu wanahitaji kuona kila mchezaji anafuata taratibu na kanuni za klabu hiyo kikamilifu.

"Tulisikiliza hoja za pande zote mbili, tulikutana na Lamine wakati timu mkoani, baadaye tukazungumza na kocha (Nabi), hivyo tumefanyia kazi hoja zao na sasa mambo safi na Lamine yuko kambini Avic Town, Kigamboni, akiendelea na mazoezi kwa ajili ya michezo yetu ijayo," Mfikirwa amenukuliwa na gazeti la Nipashe

Kutokana na adhabu aliyokuwa anaitumikia, Lamine alikosa mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC na JKT Tanzania pamoja na mchezo wa hatua ya robo fainali mashindano ya Kombe la FA dhidi ya Mwadui Fc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’