Nahodha wa zamani Stars na Yanga, Ally Mayay Tembele ameenguliwa kwenye uchaguzi wa Chama cha Wachezaji Tanzania (SPUTANZA) kwa madai ya kutokidhi vigezo vya Katiba
Taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyotolewa jana, ilibainisha kuwa Mayay ameenguliwa kwa sababu hajatelekeza Ibara ya 27 (6) ya Katiba ya SPUTANZA
Kamati hiyo imempitisha mchezaji mwingine wa zamani wa Yanga, Abeid Mohamed Mziba pekee kuwania Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kupitia SPUTANZA
Mayay ameeleza kushangazwa na kuenguliwa kwake akiwa hafahamu ni vigezo gani hajakidhi
Ikumbukwe Mayay aligombea Urais wa TFF katika uchaguzi uliopita ambao Wallace Karia alishinda
Wadadisi wa mambo wanasema uchaguzi wa TFF unakaribia mwezi August, haya ni maandalizi ya ushindi wa kimbunga!