Lwandamina atua na majina ya viungo sita

Admin By Admin
•
7 Jul 2017
Lwandamina atua na majina ya viungo sita
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amewasili tangu Jumatatu iliyopita kutoka Zambia alikokuwa mapumziko ulipomalizika msimu wa VPL 2016-17 ambao Yanga ilitwaa taji kwa mara ya tatu mfululizo.

Wakati akiwa likizo kocha huyo alikuwa akiendelea kutafuta vichwa vya maana kuvileta jangwani.

Usajili wa mwaka huu Yanga umefanywa kwa kufuata mapendekezo ya kocha huyo kwa asilimia 100 na mwenyewe akapewa jukumu maalum la kusaka viungo watakaoipaisha Yanga kwenye michuano ya Kimataifa.

Yanga imekuwa ikiteseka sana kwenye nafasi ya kiungo mkabaji, Na ni ukweli usiopingika kuwa tangu kuondoka kwa Athumani Iddi 'Chuji' Yanga haijawahi kupata mbadala wake.

Frank Domayo ambaye baadae alitimkia Azam FC alijaribu tu.

Akizungumza na gazeti moja la michezo, Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Yanga, Hussein Nyika amesema Yanga imedhamiria kuunda kikosi kitakachokuwa tishio kwenye michuano ya Afrika.

Usajili wa mwaka huu hauangalii VPL pekee, pia kuhakikisha Yanga haiwi msindikizaji kwenye michuano ya Afrika msimu ujao.

“Tunaendelea na usajili kikubwa tunacholenga sasa na kiukweli tunataka kufanya mapinduzi makubwa ni katika safu ya kiungo ambayo kwa muda mrefu tumekuwa ikitusumbua kwa namna moja ama nyingine,” amesema.

“Tulichofanya kama kamati tumekubaliana kocha ndiye aamue ni mchezaji gani anamtaka, tumefanikiwa kumsafirisha ili akafuatilie viwango mbalimbali vya wachezaji tunaowataka na mpaka sasa ana majina sita ya viungo tofauti katika meza yake.

“Majina hayo atayaamua yeye ni wachezaji gani anaona ni mwafaka kwetu ili sisi uongozi tumalizane nao baada ya kupata baraka zote kutoka kwake.

"Tunataka kuona kama tunamsajili kiungo mkabaji awe mtu wa kazi kweli lakini kama tukisajili kiungo mchezeshaji awe ni mtu anayejua sawasawa,” alisisitiza lakini hakuweka wazi ni wachezaji gani kwa madai kwamba atakuwa anauza silaha.

“Katika hayo majina sita mapya tunataka watu wanne wa uhakika ambao, anayecheza kiraka atakuwa na nafasi kubwa ya kusajiliwa.”

Miongoni mwa majina yanayotajwatajwa ni pamoja na Kabamba Tshishimbi (DR Congo), Cleatus Chota Chama (Zambia) na Fernando Bongnyang (Cameroon).

Pia yumo Zimiselem Moyo(Zimbabwe) anayechezea ZANACO, Mabingwa wa Zambia na kinara wa kundi D michuano klabu bingwa barani Afrika
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →