Washambuliaji Michael Sarpong na Fiston Abdulrazak wana mechi tano za kutetea hatma yao kuendelea kubaki Jangwani
Wiki iliyopita Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said alibainisha kuwa hawataendelea kubaki na wachezaji ambao wameshindwa kuisaidia timu
Sarpong na Fiston ni nyota wa kigeni ambao kama itapigwa kura ya maoni kwa mashabiki wa Yanga, wengi watapendekeza waachwe
Sarpong amefunga mabao manne kwenye ligi wakati Fiston aliyetua katika usajili wa dirisha dogo, amefunga bao moja tu

Fiston alisaini mkataba wa miezi sita ambao unamalizika mwishoni mwa msimu wakati Sarpong yeye alisaini mkataba wa miaka miwili
Hata hivyo Yanga ina ofa mkononi kwa ajili ya Sarpong anayewaniwa na moja ya timu kutoka bara Asia
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kuhusu hatma yao lakini ni wazi kama watapata nafasi katika michezo iliyobaki, wanapaswa kufanya kitu tofauti kuwashawishi Wananchi