Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema wanaendelea na program za mazoezi licha ya baadhi ya wachezaji kukosekana kutokana na majukumu ya timu ya Taifa
Baada ya mapumziko ya wikiendi, Yanga ilirejea mazoezini jana kuendelea na kujiandaa na michezo ya lala salama ligi kuu ya Vodacom pamoja na mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Biashara United
Hafidh amesema wana upungufu wa wachezaji kutokana na kukosekana kwa wachezaji waliokwenda kutimiza majukumu ya timu za Taifa huku baadhi ya nyota wakiwa majeruhi
ADVERTISE HERE