Mshambuliaji wa Mbeya City Kibu Denis anakaribia kuwa Mwananchi
Habari za uhakika kutoka chanzo makini ndani ya uongozi wa Yanga, zimethibitisha kuwa mwamba huyu atavaa uzi wa njano na kijani msimu ujao
Kibu ni mmoja wa washambuliaji wazawa waliofanya vizuri sana msimu huu, akiifungia Mbeya City mabao saba
Yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ambacho kesho Jumapili kitashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Malawi, mchezo wa Kimataifa wa kirafiki
Inaelezwa usajili wake uko katika hatua za mwisho kukamilishwa
ADVERTISE HERE