Kamati ya mabadiliko Yanga kuanza kazi Januari 2018

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
27 Dec 2017
Kamati ya mabadiliko Yanga kuanza kazi Januari 2018
Kamati maalum iliyoundwa na uongozi wa Klabu ya Yanga kwa ajili ya kusimamia na kuendesha mchakato mzima wa mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu hiyo, imepanga kukutana mwezi ujao kuanza kazi.

Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, chini ya Kaimu Mwenyekiti wake, Clemence Sanga, iliunda kamati hiyo kuratibu mabadiliko hayo ya uendeshwaji wakifuata nyayo za watani zao, Simba.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Alex Mgongolwa, amebainisha kuwa Kamati imepanga kukutana mara baada ya kipindi hiki cha sikukuu za mwishoni mwa mwaka.

"Tutaanza rasmi kazi baada ya sikukuu ya mwaka mpya, cha kwanza tutakutana kama kamati kupanga nini tutakachoanza nacho kuhakikisha tunafikia malengo yaliyowekwa," alisema Mgongolwa.

Aidha, alisema kuwa kamati yake itahakikisha inatafuta njia ya kuwafikia Wanayanga wote kupata maoni yao juu ya mabadiliko na mfumo sahihi wa kufuatwa ndani ya klabu hiyo.

“Wanachama ndio wenye maamuzi, sisi kama kamati tumepewa tu majukumu yakuhakikisha tunasimamia mabadiliko haya, soka la sasa hivi linaendeshwa kisasa, hivyo ni lazima kuwapo na njia nzuri ya kuiongoza klabu,” aliongezea kusema Mgongolwa.

Alisema wanaamini mchakato huo hautachukua muda mrefu kukamilika.

Simba, ambayo nayo inadhaminiwa na SportPesa, ilipitisha mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu hiyo mwezi uliopita baada ya mchakato wa mabadiliko uliodumu kwa mwaka mmoja ambapo kwa sasa timu hiyo itakuwa ikiendeshwa kwa hisa huku mwanachama Mohamed "Mo" Dewji akinunua hisa asilimia 50 za klabu hiyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →