Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Kelvin Yondani wanatarajiwa kuukosa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 12 dhidi ya Mbao FC, Disemba 31, 2017.
Licha ya kuanza mazoezi mepesi, wachezaji hao bado hawako timilifu kuweza kurejea dimbani kulingana na daktari wa Yanga, Dk Edward Bavu.
Obrey Chirwa atakosa mchezo huo baada ya kuchelewa kurudi kutoka kwao Zambia alikokwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia.
Aidha imefahamika msiba aliopata kocha Mkuu George Lwandamina huko Zambia umemlazimu Chirwa abaki huko kwa siku kadhaa kumpa 'sapoti'
Mshambuliaji Ibrahim Ajib Migomba nae atakosekana katika mchezo huo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Huenda Yanga ikatumia kikosi chake kilichopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Reha FC kwenye kombe la FA Jumapili iliyopita kuikabili Mbao FC.

ADVERTISE HERE