Vipi arudishwe nyumbani?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jun 2021
Vipi arudishwe nyumbani?

Mlinda lango wa Mwadui Fc Mussa Mbisa anahusishwa kuwa kwenye mpango wa usajili wa Yanga

Mbisa ni mmoja wa wachezaji waliolelewa na Yanga katika kikosi cha vijana (Yanga B) kabla ya kuondoka kwenda kusaka changamoto nje

Pamoja na Mwadui Fc kuteremka daraja, Mbisa amekuwa kwenye kiwango bora, juzi akifanya kazi kubwa katika mchezo dhidi ya Yanga ambao Wananchi walishinda mabao 3-2

Katika mchezo huo, Mbisa aliokoa mkwaju wa penati huku akiwapa wakati mgumu washambuliaji wa Yanga kufunga mabao

Baada ya mchezo huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, alionekana akimpongeza kwa mchezo mzuri lakini pia akionekana kumwambia jambo

Yanga inatarajiwa kuongeza mlinda lango mwingine. Mkenya Farouk Shikhalo ambaye mkataba wake unamalizika, bado hajapewa mkataba mpya

Aidha bado kuna sintofahamu juu ya Metacha Mnata ambaye alisimamishwa kufuatia tukio la kuwatusi mashabiki baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’