Baada ya mchakato wa Mabadiliko kukamilika, Yanga itaunda kampuni ambayo itamilikiwa na klabu kwa asilimia 100%
Baadae Yanga itauza asilimia 49% ya hisa za kampuni hiyo huku asilimia 51% zikiendelea kubaki mikononi mwa Wanachama
Hisa zitauzwa kwa Wawekezaji wasiozidi wanne na wasiopungua watatu hivyo kuondoa uwezekano wa Mwekezaji mmoja kumiliki kila kitu kama ilivyo kwa watani zetu
Safari ya Yanga mpya itaanza Jumapili, Juni 27 baada ya Mkutano Mkuu wa Wanachama ambao watafanya marekebisho ya Katiba kabla kuidhinisha muundo huo mpya
ADVERTISE HERE