Yanga yakwea pipa kuifuata Mbao FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
29 Dec 2017
Yanga yakwea pipa kuifuata Mbao FC
Wakati kikosi cha Yanga leo kikitarajia kukwea ‘Pipa’ kuifuata Mbao FC jijini Mwanza, Kikosi hicho cha Kocha George Lwandamina kipo kwenye ‘mtihani’ kutokana na kuwakosa washambuliaji wake nyota, Ibrahim Ajibu na Obbrey Chirwa.

Chirwa peke yake amefunga mabao sita huku Ajibu aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Simba amefunga mabao matano na kuisaidi Yanga kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikizidiwa kwa pointi mbili na vinara Simba.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Mkwasa, aliiambia Nipashe kuwa nyota hao hawataondoka na timu leo kwa kuwa Ajibu anatumikia kadi tatu za njano huku Chirwa bado akiwa kwao Zambia.

Aidha, kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa, alisema kuwa kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo kwao katika mchezo wao huo wa Jumapili lakini lazima wapambane kupata ushindi.

“Hatutakuwa nao, ni pigo kwa sababu wamekuwa na mchango mkubwa msimu huu, lakini lazima tujipange na tupambane kupata ushindi,” alisema Nsajigwa.

Mbali na kuwakosa nyota hao, Yanga pia itamkosa beki wake ‘kisiki’ Kelvin Yondani ambaye ni majeruhi huku pia ikiendelea kukosa huduma ya kiungo Thaban Kamusoko na Donald Ngoma mabo bado hawajapona majeraha yao.

Yanga itakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Mbao ambao wamekuwa wakiwasumbua wanapokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa CCM Kirumba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →