Yanga imejipanga kuondoka na alama zote tatu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya watani zao Simba ambao utapigwa Jumamosi Julai 03 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Injinia Hersi Said amesema wana wachezaji bora, wapambanaji na hawajawahi kuwa na hofu dhidi ya timu yoyote

"Tumejiandaa vizuri, sisi ni klabu ya mpira hatuna chochote cha kufanya zaidi ya biashara ya mpira kwa hiyo Jumamosi panapo majaaliwa tutakuwa uwanjani kupambana na Simba"
"Tumeandaa timu vizuri bila shaka tutachukua pointi tatu. Hatujawahi kuwa na hofu na kikosi chochote, timu yetu ni nzuri, tuna vijana wanaopambana na watatupa matoke,"alisema Injinia Hersi
"Sisi tunawaamini sana vijana wetu ambao wanavaa jezi ya Yanga, hatujawahi kuwa na mashaka nao"
"Ukiangalia rekodi, msimu huu tumekutana mara mbili, moja tumetoka sare, mechi nyingine tukawafunga kule visiwani Zanzibar"
"Kama klabu hatukuwahi kutoa taarifa yoyote iliyosema hatupeleki timu uwanjani Julai 3, nashangaa hizi taarifa zinatoka wapi"
"Kazi yetu ni mpira na hakuna namna tutazuia mpira usichezwe. Kwa hiyo Julai 3 tutapeleka timu, Julai 25 tutapeleka timu, hatujawahi kukimbia mechi"