Mwishoni mwa wiki Jumamosi, Julai 03 2021 Wananchi watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili watani zao Simba katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya 'fitna' zilizofanyika May 08 na kupelekea mchezo wa awali kuahirishwa, bila ya kinyongo, Yanga imekubali kucheza mchezo siku ya Jumamosi
Utakuwa ni mchezo wa tatu baina ya timu hizo msimu huu ambapo michezo miwili iliyopita, Yanga ilishinda mmoja na kutoka sare mmoja
Mchezo wa duru ya kwanza kwenye ligi ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Simba wakisawazisha jioooni
Watani hao wa jadi wakakutana tena fainali ya Mapinduzi kule visiwani Zanzibar mwanzoni mwa mwaka huu na Yanga kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati
Huu ni msimu wa tatu Simba haijapata ushindi dhidi ya Yanga kwenye ligi
Ushindi wa mwisho waliopata ilikuwa msimu wa 2018-19, Simba ikishinda bao 1-0
Michezo mitatu iliyopita (kwenye ligi) Yanga imeshinda mchezo mmoja na mingine miwili kumalizika kwa matokeo ya sare
Takwimu za jumla bado zinaibeba Yanga kwani wamehinda michezo 37 dhidi ya michezo 31 ambayo Simba wameshinda
Wananchi wao hawana maneno mengi lakini kazi yao inaonekana uwanjani