Mchezo wa kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, fundi Saido Ntibazonkiza alishiriki kikamilifu kuipa Yanga ubingwa wa michuano hiyo ambapo mkwaju wa penati ya mwisho ulipeleka shangwe Jangwani
Panapo majaaliwa, Jumamosi hii atakuwepo pale uwanja wa Benjamin Mkapa kuwapa furaha mashabiki wa Yanga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba
Saido ni mchezaji wa mechi kubwa, huyu mwamba ameng'ara sana katika mechi kubwa tangu akiwa anacheza ligi kuu kule Ufaransa na hata kwenye timu ya Taifa
Tangu alipotua Yanga mwezi Disemba, Saido amekuwa mchezaji mwenye mchango mkubwa akiweka kambani mabao manne na kutoa pasi tano za mabao
Kama sio majeraha yanayomuweka nje mara kwa mara pengine angekuwa na takwimu za kutisha
ADVERTISE HERE