Beki Abdallah Shaibu 'Ninja' amerejea kikosini akiwa na 'mzuka mwingi' kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi, Julai 03 uwanja wa Benjamin Mkapa
Ninja atakuwa tayari kushuka dimbani kuikabili Simba kama itampendeza kocha Nasreddine Nabi
Wengi wanakumbuka shoo yake ya kibabe kule visiwani Zanzibar ambapo katika mchezo wa fainali dhidi ya Simba aliwadhibiti vyema washambuliaji wa Simba akishirikiana vyema na Said Juma Makapu
Katika mchezo ule, Simba hawakupata 'shot on target' yoyote, Ninja aliwaweka mfuko Meddie Kagere na Chris Mugalu
Wananchi wanaisubiri hiyo Jumamosi ili wawafunge watu 'midomo'
ADVERTISE HERE