Kambi Yanga bado

Admin By Admin
β€’
7 Jul 2017
Kambi Yanga bado
Yanga bado haijaanza maandalizi ya msimu mpya wa VPL, 2017-18 licha ya taarifa za awali kubainisha kuwa kikosi kingeingia kambini Jumanne na baadae jana Alhamisi.

Kocha Mkuu George Lwandamina tayari yuko jijini Dar es salaam hivyo tunatumaini wiki ijayo timu itaanza maandalizi.

Pia uongozi unataka kumalizana kabisa zoezi la usajili ili wachezaji wote waanze maandalizi pamoja. Hilo ni jambo la msingi sana.

Wakati akimtambulisha Ajib juzi, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa alisema zoezi la usajili linakamilika wiki ijayo.

Yanga inahitaji kuanza maandalizi mapema kwani mchezo wake wa kwanza kabla ya ligi kuanza ni dhidi ya Simba katika mchezo wa ngao ya Jamii unaotarajiwa kupigwa Agosti 19.

Baadhi ya timu zilizoanza maandalizi ya msimu mpya ni Azam FC ambayo iko nchini Rwanda pia Simba imeanza jana Alhamisi.

Singida United imesafiri kwenda Mwanza jana Alhamisi kuanza maandalizi ya msimu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’