Bado wamepigwa na butwaa juu ya kilichowakuta uwanja wa Benjamin Mkapa jana baada ya kuchezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Wananchi, Yanga
Huu ni msimu wa pili mfululizo Simba 'wanatepeta' mbele ya Yanga licha ya tambo nyiiingi nje ya uwanja
Ni kipigo cha pili mwaka huu baada ya kichezea kichapo kule visiwani Zanzibar kwenye mchezo wa fainali kombe la Mapinduzi
Walipofungwa Zanzibar walidai wachezaji wao muhimu hawakuwepo lakini jana wamekosa sababu kwani hakuna aliyekosekana
Marehemu Dk Shika (Mzee wa mia tisa itapendeza zaidi) alikuwa na msemo wake akisema 'kidogo kidogo tutaelewana tu'
Wataelewa tu kuwa Yanga ndio mbabe wa soka hapa Tanzania, historia ilishaandikwa na itaendelea kuwa hivyo kwa miaka mingi



Yanga haihitaji wachezaji maalum kucheza mechi ya dabi. Yeyote anayepewa nafasi kuitetea chapa ya Yanga atafanya hivyo kwa moyo mmoja
Yaani jana hata kama Kocha Nasreddine Nabi angeamua kuingiza uwanjani kile kikosi cha U20 kilichocheza fainali ya ligi ya vijana dhidi ya Mtibwa Sugar, wasingetoka pia!
Wachezaji wa Yanga wanajua thamani ya kucheza katika klabu hiyo yenye historia kubwa Tanzania na barani Afrika