Baada ya mchezo dhidi ya Simba ambao Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0, jina la Mzee Mpili lilitawala sana kwenye vyombo vya habari
Ni kutokana na kauli zake alizokuwa akitoa kabla ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa juzi
Yale aliyoyasema kuhusu mchezo yalitimia, na haishangazi baadhi ya mashabiki wa Simba kuamini yeye alikuwa 'chachu' ya ushindi wa Yanga
Walichofahamu Mzee Mpili alitimiza wajibu wake kama Mzee wa Yanga, aliwahamasisha vijana nao wakapambana ipasavyo
Sasa amesema anatangulia mkoani Kigoma mapema, wafahamu kabisa watamkuta mwisho wa reli
Wananchi wanasema juzi walikuwa wakifanya mazoezi tu, mechi wataenda kucheza tarehe 25 Kigomaaa
ADVERTISE HERE