Tunaendelea kujenga timu imara - Nugaz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jul 2021
Tunaendelea kujenga timu imara - Nugaz

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema pamoja na mafanikio yanayoanza kuonekana baada ya uwekezaji wa GSM, Yanga bado inaendelea kuimarishwa

Nugaz amewataka wapenzi na wanachama wa Yanga waendelee kuiunga mkono timu yao kwani furaha ya kweli wanakaribia kuipata

"Bado hatujafika pale tunapopataka, yani kuna sehemu tukifika tutasema sasa tupo timamu. Wanachama na Mashabiki wa Yanga waendelee kutuunga mkono, mambo mazuri zaidi yanakuja," alisema

Akizungumzia mchezo dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa Benjamini Mkapa juzi Jumamosi na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Nugaz amesema ari, maarifa na upambanaji wa wachezaji vilipelekea kupatikana ushindi katika mchezo huo

Amesema Yanga hawakuwa na hofu kabisa kuelekea mchezo huo kwani walifahamu wataibuka na ushindi

"Simba wana kikosi kipana kwa mtazamo wao lakini sio kwetu, tuliwazidi kila kitu.Sisi tuna wachezaji ambao ukiwatuma kazi wanaenda kuifanya. Kama marefa wanachezesha kwa haki hata tukicheza nao mechi 60 tutawafunga," alitamba Nugaz

"Kocha wetu (Nabi) ni Mwalimu wa daraja la juu sana, ana upeo mkubwa, anajua madhaifu na uimara wa kila mchezaji na anajua kuwatumia vizuri. Watu hawakujua kama Zawadi Mauya anaweza kupangwa pamoja na Feisal na Mukoko"

Baada ya ushindi wa juzi Nugaz amesema wanajiandaa kwenda kuchukua ubingwa wa FA kule mkoani Kigoma akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Lake Tanganyika Julai 25

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’