Pamoja na kujiandaa kukamilisha msimu na mechi mbili za mwisho, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anakiandaa kikosi chake kwa ajili ya mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba
Mchezo huo utapigwa Julai 25, uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma
Yanga ilirejea kambini juzi kuendelea na maandalizi ambapo Julai 14 watacheza na Ihefu Fc na kumaliza msimu kwa kuikabili Dodoma Jiji ya mkoani Dodoma Julai 18
Hesabu za Yanga zaidi bila shaka zimeelekezwa kwenye fainali ya FA kwani huku wana nafasi ya kushinda taji
Kama wataifunga Simba, watashangilia taji la pili msimu huu baada ya kushinda kombe la Mapinduzi
Nabi amebainisha kuwa mchezo wa fainali FA utakuwa mgumu hivyo wanahitaji kujiandaa vyema kuhakikisha wanashinda
"Ni wazi mechi ijayo ya fainali itakuwa ngumu inabidi tuendelee kujipanga vizuri tukijua wazi ni mchezo ambao lazima mshindi apatikane," alisema Nabi
Adha Nabi ameeleza kuvutiwa na ushindani wa kikosi chake huku akiweka bayana kuwa msimu ujao watakuwa timu imara zaidi