Taarifa mbaya kwa wadau wa soka nchini ni kuwa klabu ya Polisi Tanzania imepata ajali leo asubuhi wakati ikitoka mazoezini kurejea kambini huko Moshi mkoani Kilimanjaro
Taarifa iliyotolewa na watu walioshuhudia ajali hiyo, imebainisha kuwa gari liliacha barabara na kugonga mti maeneo ya jirani na Kiwanda cha Sukari TTC ambako ndio Polisi Tanzania hufanyia mazoezi yao. Walikuwa njiani kurudi mjini yalipo makazi yao
Taarifa kutoka Makamu mwenyekiti wa timu ya Polisi Tanzania, Robert Munisi amesema mshambuliaji Gerald Mathias Mdamu amevunjika miguu kwenye ajali hiyo huku majeruhi wengine zaidi ya 10 wakipatiwa matibabu

Tunatoa pole kwa Polisi Tanzania kufuatia ajali hiyo. Mwenye ez Mungu awaponye majeruhi ili waweze kurejea katika majukumu yao
ADVERTISE HERE