Mimi ni Mwananchi, nitarudi siku moja - Niyonzima

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jul 2021
Mimi ni Mwananchi, nitarudi siku moja - Niyonzima

Kiungo mkongwe Haruna Niyonzima ameushukuru uongozi wa Yanga kwa kuthamini mchango wake na kumpa heshima ya kumuaga

Keshokutwa Alhamisi Yanga itacheza na Ihefu Fc katika mchezo wa ligi ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Mchezo huo utatumika kumuaga Niyonzima aliyeitumikia Yanga kwa takribani misimu sita

"Nawashukuru viongozi, Wanachama na mashabiki kwa hatua hii. Hii ni familia yangu, naamini siku moja nitarudi. Nafurahi kuona mchango wangu umethaminiwa mpaka kufikia kuagwa kwa heshima," alisema

Aidha Niyonzima amemtaja kiungo Zawadi Mauya kuwa mcheza anayemvutia zaidi ambaye anaamini ataweza kufuata nyayo zake kama ataendelea kuaminiwa

"Nafikiri wako wachezaji wengi lakini navutiwa zaidi na Mauya. Ni mchezaji ninaependa kumuangalia vile anavyocheza. Sio tu kwa sababu alifunga goli July 3, lakini namuona uwezo wake mazoezini na kwenye mechi"

Niyonzima ameshinda mataji manne ya ligi kuu akiwa na Yanga, amesema pamoja na kuondoka Yanga, ataendelea kucheza soka ambapo timu atakayojiunga nayo itafahamika baada ya msimu huu kumalizika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’