Leo kikosi cha Yanga kinafunga mwaka kwa kuivaa Mbao FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 12 mkoani Mwanza.
Yanga inahitaji kuibuka na ushindi katika mchezo huo ili iendelee kuzifukuza Simba na Azam ambazo zote zimeshinda michezo yao hivyo kuendelea kubaki nafasi za juu zikiwa na alama 26.
Mshambuliaji Amissi Tambwe anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga na ndiye aliyebeba matumaini ya WanaYanga leo.
Tangu arejee dimbani, Tambwe ameonekana kuimarika kiafya kwani ameweza kucheza michezo mitatu kwa dakika zote tisini huku akifanikiwa kufunga bao moja kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Reha FC wiki iliyopita
Kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema Yanga imedhamiria kukata ngebe za Mbao FC leo.
Mashabiki wa Mbao jijini Mwanza wamekuwa wakitamba kuwa wataendeleza rekodi ya ushindi dhidi ya Yanga kwenye dimba la CCM Kirumba.
Yanga imepoteza michezo yote iliyocheza na Mbao katika uwanja huo.
Kiungo Pius Buswita anarejea jijini Mwanza kwa mara ya kwanza kuikabili timu yake ya zamani, Mbao FC.

ADVERTISE HERE