Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said yuko nchini Morocco kwa mwaliko wa klabu ya Raja Casablanca ambayo ni mshirika wa Yanga
Akiwa nchini humo, Hersi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, alipata nafasi ya kuonana na winga wa zamani wa Yanga Saimon Msuva ambaye anacheza klabu ya Wydad Athletic pamoja na beki kisiki wa timu hiyo Cheick Ibrahim Comara
Hata hivyo Hersi amesema ilikuwa Mkutano wa kawaida na kuwa hakuna mazungumzo yoyote ya kumrudisha Msuva Yanga zaidi ya kumhamasisha ili aweze kwenda mbali zaidi
Yanga ilimuuza Msuva mwaka 2017 klabu ya Difaa El Jadida ambapo msimu uliopita alisajiliwa na mabingwa wa Morocco, Wydad Athletic
ADVERTISE HERE