Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Injinia Hersi Said yuko Morocco kufuatia Mwaliko wa klabu ya Raja Casablanca
Raja Casablanca na Yanga zina makubaliano rasmi ya kushirikiana katika masuala mbalimbali
Hersi yuko Morocco kupata uzoefu hasa upande wa miundombinu kutoka kwa wababe hao wa soka nchini Morocco
Raja ni miongoni mwa klabu zenye mafanikio makubwa barani Afrika ambapo mwaka 2012 wakiwa mabingwa wa Afrika, walishiriki michuano ya klabu bingwa ya dunia na kuweka rekodi ya kutinga fainali
Baada ya kufanya Mabadiliko ya muundo wake, Yanga inajipanga kujenga Taasisi imara ambayo inalenga mafanikio sio ya ndani tu, Kimataifa pia
Pichani juu Injinia Hersi alipokutana na Kocha Mkuu wa RS Berkane Florente Ibenge huko Morocco
Ibenge alijiunga na RS Berkane mapema mwezi huu akitokea klabu ya AS Vita
Tusisahau, Wananchi kuna mtupia mabao wanamtaka pale AS Vita...!