Je Akumu atamrithi Niyonzima Yanga?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jul 2021
Je Akumu atamrithi Niyonzima Yanga?

Baada ya kumuaga kwa heshima kiungo Haruna Niyonzima, Yanga imeanza kusaka mrithi wake

Katika hafla ya kumuaga nyota huyo raia wa Rwanda iliyofanyika baada ya mchezo dhidi ya Ihefu Fc ambao Yanga ilishinda mabao 2-0, Mwenyekiti wa mabingwa hao wa kihistoria Dk Mshndi Msolla alisema kuwa watamleta kiungo mwenye sifa na vigezo kwa kufuata mahitaji ya kocha Nasreddine Nabi

Aidha, Yanga inatarajiwa kusajili viungo wawili ambapo mwingine atachukua nafasi ya Carlinhos aliyeondoka wiki chache zilizopita

Wananchi wamejihakikishia kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao, hivyo usajili wao utazingatia wachezaji wenye uzoefu na michuano hiyo

Miongoni mwa nyota wanaotajwa kuwa wanaweza kusajiliwa kuchukua nafasi ya Niyonzima ni kiungo Mkenya Antony Akumu ambaye kwa sasa anakipiga klabu ya Kaizer Chiefs

Yanga imejipanga kuwasilisha ofa kwa Chiefs ili kumsajili kiungo huyo ambaye walijaribu kumnasa msimu uliopita bila ya mafanikio

"Tunadhani Akumu anaweza kuwa chaguo sahihi kuziba nafasi ya Niyonzima. Tunasubiri amalize majukumu ya ligi ya mabingwa na klabu yake ya Kaizer Chiefs ili tuweze kuzungumza nao," alidokeza mtoa taarifa

"Tumemfuatilia Akumu tangu alipokuwa Zambia akicheza Zesco United. Tunafahamu hana furaha pale Kaizer Chiefs kwa sababu hapati nafasi ya kucheza mara mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza. Ni mchezaji mzuri, anaweza kutusaidia kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao"

"Tunahitaji kujenga kikosi imara ili tuwe na timu yenye ushindani kwenye michuano ya ligi ya mabingwa. Tunahitaji wachezaji wenye uzoefu na michuano hiyo"

Mayele ni suala la muda tu

Katika hatua nyingine, Yanga inatajwa kumalizana na mshambuliaji wa AS Vita Fiston Kalala Mayele anayetarajiwa kuwasili nchini pamoja na Mcongomani mwenzake Shabani Djuma aliyesajiliwa kutoka klabu ya AS Vita

Mayele anatajwa kuwa ndio chaguo la kocha Nasreddine Nabi miongoni mwa washambuliaji waliokuwa wakiwaniwa na Yanga

Mshambuliaji huyo atakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Yanga kutoka klabu ya AS Vita katika kipindi cha miaka miwili baada ya usajili wa Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda na Shabani Djuma

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’