Mabingwa soka Tanzania Bara Yanga leo wameendeleza uteja dhidi ya Mbao FC kwenye dimba la CCM Kirumba baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0.
Mbao FC ilitawala mchezo huo tangu dakika ya kwanza. Kwa tathmini ya kawaida ni rahisi, Mbao FC ilistahili kuibuka na ushindi huo mnono.
Habibu Kiyombo ndiye aliyekuwa mwiba mchungu kwa Yanga kwani ndiye aliyepachika mabao yote ya Mbao kwenye kipindi cha pili.
Kiyombo ndiye kinara wa upachika mabao wa Mbao FC sasa akifikisha mabao saba, bao moja nyuma ya Emanuel Okwi wa Simba.
Licha ya kucheza pungufu takribani dakika 15 za mwisho vijana wa Mbao waliweza kulinda ushindi wao.
Yanga haikuwa na mchezo mzuri hakika ni moja ya michezo ambayo Yanga imecheza kiwango cha chini kabisa msimu huu.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Yanga msimu huu katika michezo yote na matokeo hayo yameishusha hadi nafasi ya nne baada ya Singida United kuitandika Njombe Mji mabao 3-1 hivyo kufikisha alama 23 na kupanda hadi nafasi ya tatu.
Baada ya mchezo huo Yanga inaelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi. Ligi kuu ya Vodacom itasimama kupisha michuano hiyo inayomalizika januari 13, 2018

ADVERTISE HERE