Klabu ya Horoya Ac imetangaza kufikia makubaliano na mshambuliaji Heritier Makambo juu ya kusitisha mkataba wake
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo mapema jana, imebainisha kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili
Horoya imemtakia kila la kheri Makambo katika maisha yake ya soka huko aendako
Makambo alikuwa bado na mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo
Hii ni habari njema kwa Wananchi kwani kumekuwa na jitihada za kujaribu kumrudisha mshambuliaji huyo aliyeifungia Yanga mabao 22 katika msimu mmoja aliyoitumikia
Makambo ni mmoja wa washambuliaji wanaotajwa kuwa mbioni kumalizana na Yanga
Mwingine ni mshambuliaji Fiston Mayele ambaye pia klabu ya AS Vita imethibitisha kuwa hatakuwa na timu hiyo msimu ujao
Wananchiiiii, tusubiri habari njema.......!