Leo haikuwa siku nzuri kwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jan 2018
Leo haikuwa siku nzuri kwa Yanga
Kukosekana kwa Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa kumeifanya Yanga ikose mbinu mbadala kwenye ushambuliaji dhidi ya vijana wa Mbao FC waliokuwa imara sana.

Chirwa na Ajib wana uwezo wa kukaa na mpira pamoja na mbinu za kuweza kuwatoroka walinzi wa timu pinzani na hivyo kutengeneza nafasi za kufunga mabao.

Amissi Tambwe ni mshambuliaji wa kati, ili aweze kufanya vizuri lazima apelekewa mipira huduma ambayo aliikosa leo.

Ajib ameukosa mchezo huo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano lakini si hivyo kwa Chirwa. Yeye aliamua tu kuukosa mchezo huo. Anazo sababu zake za msingi tunaziheshimu

Yanga bado inakosa mbinu mbadala hasa inapocheza kwenye viwanja vyenye changamoto ya 'pitch'.

Umiliki wa mpira pamoja na upigaji pasi ulikuwa mbovu, haijapata kutokea.

Hata hivyo vijana wa Mbao FC wanastahili pongezi kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu, Kwa mpira ule wa kushambulia kwa kasi Mbao inaweza kuifunga timu yoyote hapo CCM Kirumba.

Kwa Yanga imekuwa siku mbaya 'ofisini' na ndio matokeo ya mpira wa miguu. Kuna siku za ushindi na furaha lakini pia kuna siku za kushindwa na huzuni.

Hakuna timu iliyowahi kuwa juu bila kushuka chini. Changamoto za kupoteza michezo zinasaidia wakati mwingine kuboresha mapungufu yanayojitokeza.

Tunawapa pongezi Mbao FC kwa kutupa somo leo, tunawasubiri kwenye mchezo wa marudio katika dimba la Uhuru.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
54m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’