Wananchi wanatarajiwa kupaa mkoani Kigoma kesho Alhamisi tayari kwa mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, Julai 25 kunako uwanja wa Lake Tangayika
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema wanaendelea vyema na maandalizi kuelekea mchezo huo ambao wamepania kushinda
Amesema mchezo huo ni vita kwao, wanahitaji kushinda ili kujitwalia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa kwa nguvu zao wenyewe
Mfikirwa alisema wameamua kwenda Kigoma mapema ili wachezaji wao wapate nafasi ya kuzoea mazingira ya mji huo pamoja na kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Lake Tanganyika ambao ni mgeni kwa nyota wake
"Tunaendelea na maandalizi katika kiwango cha juu ikiwamo kuwahi kufika Kigoma mapema ili kuandaa mazingira bora ya timu, sehemu ya kufanyia mazoezi na kufikia wachezaji wetu, kwa upande wa uongozi tuna imani na vijana wetu, kikosi kipo fiti kwenda kutafuta ushindi katika fainali hiyo," alisema Mfikirwa.
Kiongozi huyo alisema wamejipanga kwenda kuendeleza rikodi ya kuwafunga wapinzani wao kwa mara ya pili katika ardhi ya Bongo.
"Siku zote tunasema kuwa fainali haichezwi bali fainali hushindwa, hivyo kuelekea katika mchezo huo, tunaenda kwa ajili ya kushinda fainali hiyo na kila kitu kinaenda vizuri na tutapata ushindi"