Pamoja na kuwa mkataba wake umemalizika, uongozi wa Yanga bado haujafanya mazungumzo na mlinda lango Metacha Mnata ili kumuongezea mkataba
Metacha alisimamishwa baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kufuatia tukio la utovu wa Nidhamu alilofanya baada ya mchezo huo
Tayari amemaliza adhabu ya kukosa michezo mitatu aliyokuwa amepewa na Bodi ya Ligi kutokana na tukio hilo
Meneja wa mchezaji huyo Jemedari Said amesema uongozi wa Yanga bado haujawasiliana nae kuzungumza hatma yake
Aidha Jemedari amethibitisha kuwa Yanga tayari imemlipa Metacha fedha za nyuma alizokuwa akidai
"Bado tunasubiri ofa kutoka kwa Yanga maana ndiyo sehemu ambayo anaweza kuonesha uwezo wake na ukaonekana zaidi ndani na nje ya Tanzania"
"Huyu ni kijana mdogo ndiyo kwanza na miaka 22 kwahiyo bado damu inachemka na anawaza mambo mengi na kilichotokea dhidi ya Mwenyekiti wa klabu tatizo limeisha hata sisi kama walezi hatukupenda kilichotokea," alisema Jemedari