Wananchi wamepania kwelikweli Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jul 2021
Wananchi wamepania kwelikweli Jumapili

Pamoja na kuwa Yanga tayari imejihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao, Wananchi wamesisitiza kuwa watahakikisha wanashinda mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, Julai 25 uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma

Yanga imewasili Kigoma mapema leo kukamilisha maandalizi yake ya mwisho kabla ya kuwakabili watani zao katika mchezo ambao kombe litakuwa uwanjani

Afisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema timu iko imara na wako Kigoma kwa kazi moja tu, kutwaa ubingwa wa michuano hiyo

Nugaz amesema wanahitaji ushindi  dhidi ya watani zao ili kujitwalia tiketi ya kushiriki mashindano ya CAF kwa nguvu zao

"Sisi tumejiandaa kikamilifu na tumekuja Kigoma kwa kazi moja tu,  kuifunga Simba na kuwa mabingwa wa FA. Tunataka kwenda Kimataifa kwa nguvu zetu, tukutane Lake Tangayika siku ya Jumapili" alitamba Nugaz

Naye mfungaji bao pekee la Yanga katika mchezo wa ligi uliopigwa Julai 03, Zawadi Mauya amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wako tayari kuwapa furaha mashabiki wao katika mchezo huo

"Sisi wachezaji tumejiandaa tuko vizuri, nawaambia mashabiki watarajie mambo makubwa kutoka kwetu kwani tumejiandaa kupata ushindi," alisema Mauya

Yanga imetua mkoani Kigoma ikiwa na msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na waandamizi wakiongozwaMwenyekiti Dk Mshindo Msolla, Kaimu Katibu Mkuu Haji Mfikirwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano Injinia Hersi Said

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
39m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’