Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza hajajumuishwa katika kikosi kilichoweka kambi mkoani Kigoma kuelekea mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba
Saido anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja aliyopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji
Aidha, Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amethibitisha kuwa mshambuliaji Fiston Abdulrazak amerejea na yuko tayari kwa mchezo huo sambamba na nahodha Lamine Moro aliyereshwa kikosini kwa mara ya kwanza katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji
Wananchi wanaendelea na maandalizi huko Kigoma kuelekea mchezo utakaopigwa Jumapili, Julai 25 katika uwanja wa Lake Tanganyika
ADVERTISE HERE