Abdallah Shaibu 'Ninja' mrithi halisi wa Cannavaro

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jan 2018
Abdallah Shaibu 'Ninja' mrithi halisi wa Cannavaro
Huenda msimu ujao Yanga isiwe na nahodha wake Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye amedhamiria kustaafu kusakata kabumbu mwishoni mwa msimu.

Cannavaro anashikilia rekodi ya kuitumikia Yanga kwa miaka 12 akimzidi Fred Mbuna aliyedumu Yanga kwa miaka 11.

Licha ya kumsajili Mcongo Fiston Kayembe Kanku wakati wa dirisha dogo la usajili, Abdallah Shaibu 'Ninja' ni beki aliyesajiliwa kutoka Jan'gombe Boys wakati wa dirisha kubwa la usajili mwezi Juni,2017.

Beki huyu ana sifa zote alizokuwa nazo Cannavaro wakati huo alipokuwa bado kijana kabisa.

Aina ya uchezaji wa Ninja huwezi kutofautisha na Cannavaro wakati mwingine kwa mbali unaweza hata ukadhani aliye dimbani ni Cannavaro kwani wanafanana mpaka vimo vyao na hata wanavyotembea/kukimbia.

Nimevutiwa na kiwango chake kwenye mchezo wa Yanga uliofunga mwaka 2017 dhidi ya Mbao FC ambapo Yanga ilichapwa mabao 2-0.

Ninja anahitaji kupewa nafasi zaidi ya kucheza ili aongeze kujiamini na kumkomaza zaidi.

Hakuna shaka, Ninja ni mmoja wa mabeki hazina wa kikosi cha Yanga.

Bila shaka benchi la ufundi litampa nafasi zaidi katika michuano ya kombe la Mapinduzi iliyoanza siku mbili zilizopita visiwani Zanzibar.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’