Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mapinduzi Balama hajaonekana kikosini kwa takribani mwaka mmoja baada ya kupata majeraha mwishoni mwa msimu wa 2019/20
Kwa wiki kadhaa Balama ameendelea kufanya program maalum ya mazoezi ili kuhakikisha anarejea uwanjani pasipo kupata madhara
Wananchi watarajie kumshuhudia dimbani kwenye michuano ya Kagame inayotarajiwa kuanza wiki ijayo jijini Dar es salaam
Yanga imethibitisha itashiriki michuano hiyo na bila shaka itawatumia baadhi ya wachezaji wapya na wale ambao wako katika mipango ya kocha Nasreddine Nabi lakini hawakupata muda wa kutosha kuonekana msimu huu
Katika michuano hiyo pia baadhi ya nyota wa kikosi cha vijana wa U20 huenda wakatumika
ADVERTISE HERE