Maisha ya Bradley yamefika tamati

Admin By Admin
β€’
8 Jul 2017
Maisha ya Bradley yamefika tamati
Wazazi wa mtoto Bradley Lowery (6) wametoa taarifa kuwa mtoto huyo amefariki dunia majira ya saa saba mchana kwa saa za Uingereza baada ya kupambana na kansa kwa miaka kadhaa.

Kwa wale wanaofuatilia ligi kuu ya Uingereza ni dhahiri waliwahi kumuona mtoto huyu dimbani hasa michezo ya Sunderland. Alikuwa shabiki mkubwa wa timu hiyo.

Matatizo yake yalimgusa aliyekuwa mshambuliaji wa Sunderland Jermain Defoe ambaye alikuwa rafiki yake mkubwa tangu msimu uliopita.



Defoe alikuwa akitumia muda mwingi kukaa na kucheza na mtoto huyo aliyekuwa na maradhi yasiyopona. Defoe alionyesha upendo wa hali ya juu kwa mtoto huyo.

Jana Alhamisi Defoe alitambulishwa na klabu yake mpya, Bournemoth, aliulizwa na wanahabari juu ya hali ya Bradley, alishindwa kuzuia machozi yaliyomtiririka mbele ya waandishi wa habari.

Kumbe madaktari wanaomtibu Bradley walishaieleza familia yake kuwa maisha ya mtoto huyo yalikuwa yamefika tamati kulikuwa hakuna namna nyingine ya kumsaidia.

Bradleya lipewa heshima ya pekaa nchini Uingereza ambapo mara ya mwisho aliiongoza dimbani timu ya Taifa ya Uingereza katika mchezo wa kusaka tiketi ya kombe la dunia dhidi ya Lithuania.



Mara kadhaa klabu ya Sunderland ilimualikwa katika dimba lake na kujuika na wachezaji wa timu hiyo wakimtumia kama balozi wao.

Kifo chake kimewahuzunisha wadau wengi wa soka duniani kwani baada ya taarifa za kifo chake kutangazwa salamu za kuomboleza zilifurika kwenye mitandao ya kijamii.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’