Yanga ina takribani wiki mbili kukamilisha usajili wa wachezaji wake watakaoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Septemba
Awamu ya kwanza ya kalenda ya usajili kwa ajili ya michuano hiyo itafungwa August 15, takribani wiki mbili zikiwa zimesalia
CAF imeruhusu usajili wa wachezaji hadi 40 wakati huu ambao bado kuna changamoto ya janga la corona
Yanga inaweza kusajili zaidi ya nyota 10 wa kigeni kwa ajili ya michuano hiyo lakini wale watakaoruhusiwa kushiriki michuano ya ndani, idadi itabaki kuwa 10
ADVERTISE HERE