Shihkalo agoma kuzungumzia hatma yake Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jul 2021
Shihkalo agoma kuzungumzia hatma yake Yanga

Mlinda lango Farouk Shikhalo raia wa Kenya ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao na Yanga imemalizika

Shikhalo alitua Yanga katika usajili wa mwaka 2019, ukiwa moja ya sajili zilizofanywa na Mwinyi Zahera wakati akiwa mkufunzi wa mabingwa hao wa kihistoria

Jana baada ya kuerejea kutoka Kigoma ambako Yanga ilipoteza mchezo wa fainali kombe la FA kwa kufungwa bao 1-0 na Simba, Shikhalo hakuwa tayarii kuweka wazi kuhusu hatma yake na Wananchi

"Mkataba wako umemalizika je utaendelea kubaki Yanga au unakwenda kusaka changamoto mpya mahali pengine?," mmoja wa wanahabari alimuuliza Shikhalo

"Kwa sasa sitopenda kulizungumzia hilo, tusubiri kwanza," alijibu Shikhalo kwa ufupi

Msimu huu eneo la golikipa lilikuwa mikononi mwa Shikhalo, Metacha Mnata na Ramadhani Kabwili

Kabwili bado ana mkataba wakati Shikhalo na Metacha Mnata wote mikataba yao imemalizika

Wakala wa Metacha Jemedari Said alithibitisha kuwa Yanga haijaonyesha nia ya kuongeza mkataba wa Metacha huku tetesi zikibainisha kuwa Wananchi hawana mpango nae

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’