Tarehe na mwezi kama wa leo alizaliwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Injinia Hersi Said ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji kampuni ya GSM
Wengi walimfahamu Hersi mwishoni mwa mwaka 2019 pale GSM ilipoingia rasmi kuisaidia Yanga katika masuala ya usajili
Kwa sasa imani kwake ni kubwa, wengi wanaridhika na kazi anayoifanya ndani ya klabu ya Yanga
Zungumzia usajili, zungumzia Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji, zungumzia kambi, hamasa na bonus za wachezaji ni miongoni mwa majukumu aliyoyafanya kwa ufanisi
Wananchi wanajivunia kuwa nae hasa wakati huu ambao timu inajipanga kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya michuano ya Kimataifa
Ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, tunamtakia kila la kheri
HAPPY BIRTHDAY HERSI
ADVERTISE HERE