Wachezaji 23 wa kikosi cha Yanga watashiriki michuano ya kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Jumapili, August 1 jijini Dar es salaam
Baada ya Yanga kuwapa wachezaji na benchi la ufundi mapumziko ya wiki mbili, kumeibuka sintofahamu juu ya kikosi kitakachoshiriki michuano ya Kagame
Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli ametoa ufafanuzi ambapo amesema nyota saba wa kikosi cha kwanza, wataungana na wachezaji 10 kutoka timu ya vijana (Yanga B) huku wachezaji wengine sita wakiwa ni wapya
"Tutakuwa na kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki Kagame Cup, wachezaji sita watakuwa ni wapya, wachezaji saba watatoka kwenye kikosi cha kwanza na wachezaji 10 ni kutoka timu ya vijana wa U20," alisema Bumbuli
Bado majina ya wachezaji sita wapya watakaoshiriki michuano hiyo hayajawekwa wazi
Yanga imepangwa kundi C na klabu za Express (mabingwa wa Uganda) na Nyasa Big Bullets kutoka nchini Malawi